Misri
|
|||
| Lugha rasmi | Kiarabu | ||
| Mji Mkuu | Cairo-Maadi | ||
| Serikali | Jamhuri | ||
| Rais | Abdel Fattah el-Sisi | ||
| Waziri Mkuu | Ibrahim Mahlab | ||
| Eneo | km² 1.002.450 | ||
| Wakazi | 88.000.000 (2015) | ||
| Wakazi kwa km² | 84 kwa jumla; katika bonde la Nile 1120 | ||
| Uhuru | 26 Julai 1952 kutoka Uingereza | ||
| Pesa | Lira au Pauni ya Misri = 100 Piaster | ||
| Wakati | UTC +2 | ||
| Wimbo ya Taifa | Biladi, Biladi, Biladi (nchi yangu) | ||
| Mahali pa Misri duniani | |||
Misri (kwa Kiarabu: مصر Masr) ni nchi ya Afrika ya Kaskazini-Mashariki.
Jiografia[hariri | hariri chanzo]
Misri imepakana na Bahari ya Mediteraneo, Israel, Eneo la mamlaka ya Palestina, ghuba ya Suez, ghuba ya Aqaba, Bahari ya Shamu, Sudan na Libya.
Rasi ya Sinai ambayo ni sehemu ya Misri huhesabiwa pengine kuwa sehemu ya bara la Asia.
Misri yenyewe ni nchi ya jangwa yenye oasisi kadhaa.
Katikati ya nchi unapita mto wa Naili kutoka Sudani upande wa kusini hadi Mediteranea upande wa kaskazini. Sehemu kubwa ya njia yake ni bonde jembamba ambalo kandokando yake kuna kilomita chache za ardhi inayomwagiliwa na kulimwa, nyuma yake ni jangwa tupu.
Takriban kilomita 250 kabla ya mdomo Naili inagawanyika katika mikono mbalimbali na kuunda delta ya mto.
Mji mkuu wa Kairo uko mwanzoni mwa eneo la delta.
Bonde la Naili pamoja na delta ni takriban asilimia 4-5 ya nchi yote na katika sehemu hiyo ndogo wanaishi asilimia 98 ya wananchi wote. Kwa hiyo Naili huitwa "Baba wa Misri" kwa maana bila mto huo pasingekuwepo taifa hili.
Historia[hariri | hariri chanzo]
Nchi hiyo ni kati ya vitovu vya ustaarabu wa binadamu, na kwa sababu hiyo inavutia watalii wengi.
Watu[hariri | hariri chanzo]
Wakazi wengi (91%) ni Wamisri asili.
Lugha rasmi ni Kiarabu Sanifu cha Kisasa, wakati wananchi wanatumia kwa kawaida aina mbalimbali za Kiarabu, hasa Kiarabu cha Kimisri (68%)
Upande wa dini, sheria zinazitambua 3 tu: Uislamu, ambao ndio dini rasmi, Ukristo na Uyahudi. Uwiano wa wafuasi wa dini hizo haujulikani vizuri, lakini Waislamu (hasa Wasunni) ni kama 90%, Wakristo (hasa Wakopti wanaoendelea kufuata Ukristo uliokuwa unatawala kabla ya Waarabu kuteka nchi katika karne ya 7) ni kama 9%, wakati Wayahudi wamehama karibu wote.
Tazama pia[hariri | hariri chanzo]
Viungo vyo nje[hariri | hariri chanzo]
- Serikali
- Egypt's Government Services Portal (Arabic, English)
- Egypt Information Portal (Arabic, English)
- Egypt Information and Decision Support Center (Arabic, English)
- Egypt State Information Services (Arabic, English, French)
- Chief of State and Cabinet Members
- Egyptian Tourist Authority
- Taarifa za jumla
- Country Profile from the BBC News
- Egypt entry at The World Factbook
- Egypt profile from Africa.com
- Misri katika Open Directory Project
- Wikimedia Atlas of Egypt
- Egypt Maps – Perry-Castañeda Library Map Collection, University of Texas at Austin
- Biashara
- Mengineyo
- History of Egypt, Chaldea, Syria, Babylonia, and Assyria in the Light of Recent Discovery by Leonard William King, at Project Gutenberg.
- Egyptian History (urdu)
- By Nile and Tigris - a narrative of journeys in Egypt and Mesopotamia on behalf of the British museum between 1886 and 1913, by Sir E. A. Wallis Budge, 1920 (DjVu and layered PDF formats)
- Napoleon on the Nile: Soldiers, Artists, and the Rediscovery of Egypt.
| Nchi za Afrika | |
|---|---|
| Afrika ya Kati (Jamhuri ya) | Afrika Kusini | Algeria | Angola | Benin | Botswana | Burkina Faso | Burundi | Cabo Verde | Chad | Cote d'Ivoire | Eritrea | Gabon | Gambia | Ghana | Guinea | Guinea Bisau | Guinea ya Ikweta | Jibuti | Kamerun | Kenya | Komori | Kongo (Jamhuri ya) | Kongo (Jamhuri ya Kidemokrasia ya) | Lesoto | Liberia | Libya | Madagaska | Malawi | Mali | Misri | Morisi (Visiwa vya) | Mauritania | Moroko | Msumbiji | Namibia | Niger | Nigeria | Rwanda | Sahara ya Magharibi | Sao Tome na Principe | Senegal | Shelisheli | Sierra Leone | Somalia | Sudan | Sudan Kusini | Tanzania | Togo | Tunisia | Uganda | Uhabeshi | Uswazi | Zambia | Zimbabwe | |
| Maeneo ya kiafrika ambayo ni sehemu za nchi nje ya Afrika | |
| Ufaransa: Mayotte · Réunion | Hispania: Visiwa vya Kanari · Ceuta · Melilla | Ureno: Visiwa vya Madeira | Uingereza: · Kisiwa cha St. Helena · Kisiwa cha Diego Garcia | |
| Makala hii kuhusu maeneo ya Afrika bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Misri kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |